ISBN: | 9781783687466 |
---|---|
Imprint: | One-Volume Commentaries |
Format: | Hardback |
Edition: | 1 |
Dimensions (mm): | 235 x 188 x 46 |
Publication Date: | 14/12/2019 |
Pages: | 1824 |
Language: | Swahili |
Ufafanuzi wa Biblia Katika Mazingira na Utamaduni wa Kiafrika
Endorsements
Msingi wa maisha ya Kikristo ni katika kulifahamu kwa usahihi Neno la Mungu. Kanisa la Afrika linakua kwa haraka sana kuliko sehemu nyingine yoyote ulimwenguni. Lakini, linakosa kitabu chenye mafafanuzi katika lugha ambayo wengi wanaielewa. Upatikanaji was kitabu hiki cha Ufafanuzi wa Biblia Katika Mazingira na Utanaduni wa Kiafrika ni hatua muhimu sana ya kihistoria kwa Kanisa la Afrika Mashariki, na mahali penqine popote kinapozungumzwa Kiswahili.
Augustino S. L. Ramadhani
Jaji Mkuu wa Tanzania
Kwa muda mrefu Wakristo wanaotumia lugha ya Kiswahili wamekuwa wakisubiri kitabu cha aina hii. Lengo la kitabu hiki ni kumsaidia msomaji kuyaelewa Maandiko Marakatifu yaani Biblia kwa kina zaidi na kwa mtazamo wa mazingira na rutamaduni wa Kiafrika. Mifano iliyotumika kuielezea Biblia imetolewa kwa tamaduni mbalimbali za hapa Afrika. Hiki ni kitabu cha kwanza cha aina yake kilichoandikwa na wataalam wa Kiafrika na katika lugha ya Kiafrika. Kimeandaliwa kwa utaalamu mkubwa na kwa kina cha mawazo.
Rev. Canon Dr. Mkunga H.P. Mtingele
Kaitibu Mkuu
Chama cha Biblia cha Tanzania
Juzuu hili la kipekee ni ishara kuu ya kukua kwa Ukristo barani Afrika. Popore pale Biblia inapopendwa na kusomwa, kitabu hiki kitawasaidia watu kuielewa na vile kuishi kulingana na Maandiko Matakatifu.
Dr. Chris J. H. Wright
Mkurugenzi wa Kimataifa,
Langham Partnership Interational